Historaia Ya Enock Sikaonga Maarufu Kama Dinho Katika Ulimwengu Wa Soka. | Tunduma City Academy

Friday, 8 September 2017

Historaia Ya Enock Sikaonga Maarufu Kama Dinho Katika Ulimwengu Wa Soka.





Marehemu Enock Sikaonga maarufu kama Dinho alipatwa na umauti tarehe 20 - 8 mwaka 2017 siku ya Jumapili majira ya saa Tisa alasiri akiwa nyumbani akiendelea bado na matibabu muhimu. Ni mara Baada ya kutoka hospitali ya Ikonda Njombe kutokana na matatizo ya Vidonda shingoni, Kuiishiwa nguvu na magonjwa nyemelezi.


Nguri huyu wa Kandanda alianza safari yake katika soka na timu ya Tunduma City Academy kwa upande wa Tanzania mwaka 2007 akiwa na umri wa miaka 10. Kiwango chake kwa wakati huo kilimruhusu kuwa katika timu ndogo ya wachezaje wenye umri na lika kama lake, ubora na ufanisi wake wa kusakata mpira ulianza kumfanya awekiungo na mtu muhimu katika timu.




Mchezaji Enock (Dinho) aliendelea kufanya mazoezi , kujiimalisha na kujiboresha zaidi iliafanikishe kile alichokikusudia. Uwezo wake ulimpelekea kushiriki katika ligi mbali mbali ikiwemo ligi za wilaya , Za mkoa , Copa Cocakola (U17) na Airtel Rising Star hata hivyo alifanikiwa kuichezea timu ya Mkoa wa Mbeya ambayo ilishiriki Mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.






Baada ya mashindano Dinho alirudi nyumbani kuendelea na shule pamoja na kuendeleza kipaji chake cha kusakata soka akizidi kujijengea jina na heshima kwa kila mtu kupitia ligi za Tunduma na Zambia. Mara baada yakuhitimu shule alisajiliwa na Timu ya The Green kwa ajili ya kuichezea katika ligi ya daraja la tatu ngazi ya mkoa.



Hata hivyo Enock Sikaonga kwa ubora aliojijengea ulimfanya asajiliwe na timu ya Kapili Loket iliyopo Zambia mara baada ya kuachana na The Green na huko ndiko Maradhi ya kiafya yalianza kumsumbua. Bila kupoteza muda mchezaji huyo alichukua uamuzi wa kurudi nyumbani kwa uangalizi zaidi.






Kupitia Timu yake ya Tunduma city iliyoshirikiana na viongozi, wachezaji , wadau na wapenda kandanda na Timu zote za Tunduma zilizokuwa karibu yetu kuhakikisha Mchezaji Dinho anapata tiba bila kujali gharama. Hata hivyo marehemu Enock alitibiwa na Hospitali ya Molevyani - Tunduma, Roma-Tunduma, Rufa – Mbeya na Ikonda – Njombe.



Baada ya matibabu na kurudi nyumbani akiwa katika hali ya kutia Moyo wa kulejea katika afya yake lakini Nguvu za kuhimili maumivu zilipotea, Pumzi yake ilikata, Moyo wake ulisimama hakuna aliyeamini kwasababu kumbukumbe alizoziweka machoni pa watu ni ucheshi wake, uwezo wake na Moyo wake wa kujari.

0 comments:

Post a Comment